Michezo

Dirisha la usajili kufunguliwa Juni 15 – TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza kufungua dirisha la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa mashindano wa 2017/2018.

Dirisha hilo linafunguliwa Juni 15, mwaka huu na litafungwa Agosti 6, mwaka huu hivyo kila timu inayoshiriki michuano tajawa hapo juu, inaarifiwa kufuata kalenda hiyo ambayo tunaitangaza sasa.

Tahadhali, hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa timu ambazo hazitakamilisha usajili kama ilivyotokea msimu uliopita kwa baadhi ya timu kushindwa kufanya kusajili kwa wakati na dirisha likafungwa.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents