Habari

Dj Aaron aeleza ujio wa ‘All-stars Students Awards

Dj wa zamani wa Clouds FM, Aaron, ameanzisha kile alichokiita All-stars Students Awards.

vlcsnap-2016-05-05-13h26m40s122
DJ Aaron akiongea kwenye kipindi cha Morning Trumpet cha Azam TV

Hizo ni tuzo zitakazotolewa kwa wanafunzi wa shule za Afrika Mashariki.
Alhamis hii Dj Aaron alialikwa kwenye kipindi cha Morning Trumpet cha Azam TV kuongelea tuzo hizo zitakazofanyika jijini Dar es Salaam.

vlcsnap-2016-05-05-13h29m38s89

Aaron amesema tuzo hizo zina dhumuni la kuwapa hamasa wanafunzi wa shule za Afrika Mashariki. Tuzo hizo zitatolewa kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne na sita.

Masomo yakayotolewa tuzo ni Kiswahili, Hesabu, Fizikia, Kemia, Bailojia na Kiingereza. Mchakato wa tuzo utaanza katikati ya mwezi wa sita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents