Michezo

Djibril Cisse atangaza kustaafu soka huku machozi yakimtoka

Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa ambaye alikuwa haishi vituko na aliyewahi kuichezea klabu ya Liverpool ya Uingereza, Djibril Cisse, October 20 amefanya maamuzi ambayo wanasoka wengi huyafanya wanapoona muda umefika.

2D92773D00000578-0-image-a-1_1445296416511

Cisse ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 34. Uamuzi wake wa kustaafu soka haukuwa rahisi kwani staa huyo aliutangaza huku machozi yakimtoka katika mahojiano ya TV.

05A1892A0000044D-0-image-a-9_1445298153454

Atakumbukwa zaidi katika ulimwengu wa soka kwa kuisaidia Liverpool kutwaa taji la ligi ya mabingwa wa Ulaya. Lakini pia amewahi kutwaa tuzo ya kiatu cha dhahabu mara mbili akiwa Ufaransa na Ugiriki.

Staa huyo wa soka amewahi kucheza katika vilabu 12 vya soka vikiwemo Liverpool, Sunderland na QPR.

Cisse ambaye ametangaza maamuzi hayo huku nafsi yake ikiwa bado inatamani kuendelea kucheza soka, amekubali yaishe kutokana na umri kumtupa mkono.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents