Michezo

Droo ya Uefa Champions League yatishia watu

Drop ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajiwa kufanyika leo sea 8:00 chana kule Nyon, Uswisi ambapo macho na masikio yote yatakuwa huko kujua nani atapangwa na nani.

Arsenal na Man City ndio time pekee kutoka England ambazo zimesalia kwenye hatua hiyo. Hispania ndio Nchi iliyoingiza timu nyingi zaidi kwenye hatua hiyo katika michuano ya mwaka huu ikifanikiwa  kuziingiza Real Madrid na Barcelona ambazo zote zilimaliza hatua ya makundi zikiwa vinara.

Ujerumani pia imeingiza time mbili sawa na England ambazo ni Bayern Munich na Borussia Dortmund ambapo kumekuwa na utabiri kwamba straika wa Bayern Munich, Harry Kane huenda akarejea tena nchini England akiwa na Munich kutokana na droo hiyo. Ufaransa imeingiza timu moja tu PSG.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents