Dubai yazindua jengo lingine refu zaidi duniani
Dubai inakuwa ni sehemu pekee duniani ambayo ina majengo marefu zaidi duniani na hii ni baada ya jana Jumapili Februari 11, 2018 kuzindua jengo la Gevora Hotel towers.
Jengo hilo lenye ghorofa 75 na urefu wa mita 356 kwenda juu linakuwa ndiyo jengo la Hoteli refu zaidi duniani.
Hata hivyo, rekodi ya jengo refu la hoteli duniani ilikuwa inashikiliwa na Dubai yenyewe ambapo jengo la hoteli la JW Mariott Marquis ambalo limezidiwa mita moja tu na jengo jipya la Genova Hotel ndio lilikuwa linashikilia rekodi hiyo.
Jengo hilo la Hoteli ya Genova ina vyumba 528 na kuna klabu kubwa 5 na swimming pool na migahawa mikubwa 30.
Dubai ndiyo sehemu mpaka sasa inayoongoza kuwa na jengo refu zaidi duniani la Burj Khalifa lenye urefu wa mita 828.
Kwa mujibu wa mtandao wa Emirates 24/7 hoteli hiyo litaanza kupokea wageni kuanzia jumatatu ya wiki lijalo.