Habari

El Salvador: Wanajeshi wavamia Bunge kushinikiza kupitishwa kwa muswada wao

Wanajeshi na maafisa wa polisi waliojihami nchini El Salvador wamevamia bunge, wakitaka kuidhinishwa kwa mkopo wa dola milioni 109 ili kuwanunulia vifaa vya kukabiliana na uhalifu.

Wanajeshi waliojihami: Walivamia bunge nchini El Salvador

Waliingia katika jengo la bunge wakati rais Nayib Bukele alipokuwa anakaribia kuwahutubia wabunge .

Siku ya Ijumaa aliwapatia siku saba za kuunga mkono mpango wake wa kuchukua mkopo. Viongozi wa upinzani walitaja uvamizi huo wa wanajeshi bungeni kuwa kama kitendo cha kutishia.

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2017, taifa hilo lina idadi ya watu milioni 6.378

Rais Bukele ambaye alichukua mamlaka mnamo mwezi Juni 2019 , anataka kutumia mkopo huo kuimarisha vifaa vya maafisa wa polisi na wanajeshi katika vita dhidi ya uhalifu.

Taifa la El salvador lina viwango vya juu vya mauaji duniani. Ghasia nyingi hutekelezwa na magenge ya uhalifu ambayo hufanya kazi katika eneo la Marekani ya kati.

El Salvador's President Nayib Bukele addresses his supporters outside the parliament building in San Salvador. Photo: 9 February 2020Rais Nayib BukeleĀ 

Ameahidi kukabiliana na ghasia zinazotekelezwa na wahalifu pamoja na ufisadi katika taifa hilo lenye viwango vya juu vya umasikini.

Siku ya Jumapili , mamia ya watu walikongamana nje ya bunge katika mji mkuu wa San Salvador kuunga mkono mpango wa usalama wa rais.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents