Burudani

Emmanuel Mbasha apewa dhamana, kesi yake kusomwa tena July 17

Mume wa muimbaji wa muziki wa injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha amepewa dhamana. Mbasha aliyependa kizimbani juzi alikana mashtaka mawili yanayomkabali likiwemo la kumbaka shemeji yake.

1911114_507199476058710_1063991907_o

Mbasha ambaye pia ni muimbaji wa muziki huo alifikishwa leo katika wilaya ya Ilala ambapo kama ilivyokuwa Jumanne hii alisomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago. Kwa mujibu wa wakili wa serikali, Nassoro Katuga Mbasha alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.

Katika shitaka la kwanza, Mei 23, 2014, kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake.Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, 2014 kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).

Kwa mujibu wa hakimu, Ili kupata dhamana, Mbasha alitakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya shilingi milioni 5. Atapanda tena kizimbani July 17.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents