Burudani

#Tuzozawatu Special: Nisher apanga kutafuta suluhisho la wasanii kupenda kushoot video nje ya nchi

Zikiwa zimesalia siku 8 tu hadi kufika siku ya utoaji wa tuzo za watu utakaofanyika June 27, tunakuleta karibu na nominees mbalimbali walioingia fainali, ambao watakueleza kuhusu kazi zilizowafanya watajwe, masuala mengine kuhusu kazi zao na jinsi walivyozichukulia tuzo za watu baada ya kutajwa.

10174894_637762542971975_4790571488981251870_n

Leo tumepiga story na Nisher aliyetajwa kuwania kipengele cha muongozaji wa video za muziki zinazopendwa.

Kuhusu kushoot video ya wimbo wa Ben Pol ‘Unanichora

Video iko tofauti kidogo, sijajua mashabiki wangu watasemaje. Wimbo wa Uninichora jinsi ambavyo niliweza kukaa na Ben Pol tukaongea, nilimuuliza alipokuwa anautunga huu wimbo haya maneno na hii hisia ilikuwa inatoka wapi. Kwahiyo inaonekana kama ilikuwa inatoka kwenye sehemu iliyoumia fulani, sehemu ya moyo wake ambayo imepondeka yaani imeumizwa na kitu fulani. Kwahiyo video pia ndivyo inavyoonekana, inaonekana ni mtu aliyeumia, kuna scene inaonekana anakunywa kama whisky hivi, kuna scene demu wake anadanganywa na mademu wengine wanamletea marafiki wengine, yaani iko tofauti sana.

Kuhusu sababu zilizofanya awe na mashabiki wake mwenyewe wanaosubiri video anaziongoza kwa hamu

Mimi tangu zamani nilikuwa napenda sana social networks, nilikuwa napenda sana kukaa na watu kuchat nao then nilipoanza kufanya kazi hii ya directing nikajikuta kwamba hao hao watu niliokuwa nao wakati huo basi wanifuatilia kwahiyo tumekuwa karibu na imekuwa ni network kubwa ndio maana ni kama watu wamekua na mimi mrefu.

Kuhusu anajiona wapi baada ya miaka miwili kama muongozaji wa video

Kitu cha kwanza ninachotaka kufanya mara baada ya hizi tuzo (tuzo za watu) nataka nifanye research kwasababu sisi madirector wa Bongo tunakumbwa na janga dogo la wasanii kwenda kushoot kazi nje, kwahiyo mimi nataka kufanya research kwamba kuna nini labda sisi hatukijui ambacho wanakifuata kule nje. Tunawapondea labda na tunaongea maneno mengi lakini kumbe kuna kitu wamekiona kule ambacho sisi hatukijui. Nataka nijue huko nje kuna nini, nisafiri nionane na hao madirector wengine niwaulize labda ‘nini hawa jamaa wakijaga huku kwenu wanakipenda’ ili nijue jinsi ya kukuletea hicho kitu kwetu ili tuwabakize kwetu kwasababu inatuharibia soko kwa maana ya kwamba tunashindwa kuimarket Tanzania.

Kuhusu alivyochukulia kutajwa kuwania tuzo za watu

Mimi kwanza nilichanganyikiwa kwasababu sijawahi kutegemea, hakuna mwaka wowote niliwahi kutegemea watu wataniheshimu kiasi hiki. Mimi nimetoka Arusha wala nilikuwa sijulikani, nimeanza kufanya hii kazi miaka miwili iliyopita. Sasa hivi yaani director mkubwa, nafahamika. Yaani I didn’t expect this kabisa, niliona kama ni miujiza inatokea.

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents