Habari

Engen, Vivo Energy waungana kukuakibiashara

KAMPUNI maarufu za usambazaji wa nishati na vilainishi, Engen na Vivo Energy zimetangaza kuungana na hivyokutengeneza ushirika mkubwa wa usambazaji wa bidhaahizo barani Afrika.

Kwa kuungana kwao kumefanya wawe na uwezo wapamoja wa vituo vya huduma 3,900 na uwezo wa kuhifadhilita bilioni mbili katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika. Kampuni hizo zinafanya shughuli zao katika nchi 27 za Afrika.

Engen ambayo ni maarufu nchini Afrika Kusini ina vituovya huduma 1,300 katika nchi saba za Afrika, huku Vivo Energy ikiwa kampuni kubwa ya usambazaji wa mafuta navilainishi ina vituo zaidi ya 2,600 katika nchi 23wakitumia alama (nembo) ya Engen na Shell.

Katika muunganiko huo kampuni ya Petronas itauza hisazake asilimia 74 zilizopo katika kampuni ya Engen kwaVivo Energy na kampuni ya Phembani Group, mshirika wakaribu wa Petronas barani Afrika na mwenye hisa kwenyekampuni ya Engen ya B-BBEE ataendelea kuwa nauhusiano na Engen kwa kuendelea kuwekeza asilimia 21 ya biashara zake nchini Afrika Kusini.

Muunganiko huo utawanufaisha waajiriwa wa Engen ambao kupitia mpango maalumu wa asilimia tano waumiliki wa kampuni wa wafanyakazi unafanya asilimia 26 kumilikiwa na watu ambao awali hawakuwa wanatarajiwa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vivo Energy, Stan Mittelmananasema kwamba nia ya kampuni yake ni kuwekeza zaidikatika kukua kibiashara na kwamba tangu ianzishwemwaka 2011 wameongeza uwezo wao mara mbili zaidi.

Miaka minne iliyopita tulinunua soko la Engen katika nchinane za Afrika na tumeendelea kuhakikisha kwambatunakuza na tunakua kibiashara. Kumilikiwa kwa Vivo Energy kwa asilimia 100 na Vitol mwaka jana, kulifanyakampuni ikue kwa kasi zaidi. Makubaliano yatakapofikiamwisho katika utekelezaji wa kuunganika kwa Vivo Energy na Engen tutakuwa tumepiga hatua kubwa zaidi katikasoko la Afrika Kusini na masoko mengine muhimu,” alisema Mittelman.

Naye Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu wa Engen, Seelan Naidoo alisema kuunganika kwao na Vivo kunatoamwanga mpya katika utendaji wa kazi zao na hasakuendelea kuwa vinara katika soko la Afrika Kusini namataifa mengine ya Afrika.

Phuthuma Nhleko, Mwenyekiti na mwanzilishi mwenza waPhembani Group alisema wanajisifu sana kwa kuiwezeshaEngen kukua na kwamba sasa wanajisikia faharikuunganika na Vivo Energy katika ukuaji wa kampuni hizo.

Mwenyekiti wa Vivo Energy, Chris Bake amesema kwambakampuni hiyo imeendelea kufanya vyema tangukuanzishwa kwake na kwamba ina wataalamu namenejimenti imara yenye muono na ubunifu kuwezeshakukua na kuhudumia masoko yake muhimu likiwemo la Afrika Kusini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents