Michezo

England yatwaa kombe la Dunia

England imetwaa ubingwa wa Kombe la Dunia kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 baada ya kuichakaza Venezuela goli 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa jana nchini Japan.

Tokeo la picha la ENGLAND WORLD CUP WINNER U-20
Timu ya vijana chini ya miaka 20 wakishangilia ushindi wao

Ushindi huo wa England ndiyo mafanikio makubwa zaidi kwenye soka katika ngazi ya dunia tangu tangia timu ya wakubwa kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1966.

Katika mchezo huo, England imejipatia bao lake pekee kupitia kwa nyota wa klabu ya Everton, Dominic Calvert-Lewin dakika ya 35 kipindi cha kwanza, huku golikipa wake Freddie Woodman anayekipiga Newcastle United pia akiokoa mkwaju wa penati katika kipindi cha pili.

Nafasi ya mshindi wa tatu imekwenda kwa Italia iliyoshinda kwa mikwaju ya penati 4-1 dhidi ya Uruguay baada ya kutoka suluhu katika dakika 120.

Baada ya michuano hiyo kumalizika, tuzo mbalimbali zimetolewa ambapo Tuzo ya Mfungaji Bora wa michuano hiyo imekwenda kwa Riccardo ORSOLINI wa Italia aliyemaliza akiwa na mabao 5, huku golikipa wa England Freddie Woodman akichaguliwa kuwa Golikipa Bora wa mashindano.

Tuzo ya Mfungaji Bora imekwenda kwa kinda wa Liverpool aliyetokea Chelsea Dominic SOLANKE (England) huku Mexico ikishinda tuzo ya timu yenye mchezo wa kiungwana (Fair Play Award).

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents