Burudani

Exclusive: Q-Chief aelezea kusaini mkataba na kampuni mpya, majaribu, alichojifunza na ujio wake kama msanii aliyebadilika (Video)

Muimbaji mkongwe wa muziki wa Bongo Flava aliyewahi kuhit na nyimbo nyingi, Abubakar Katwila aka Q-Chief amesaini mkataba wa usimamizi na kampuni ya Apex Consultants & Associates ya QS ya Joseph Mhonda. Akiongea na Bongo5 kwenye mahojiano exclusive, Chief amesema kusaini mkataba na kampuni hiyo kumempa matumaini mapya baada ya kuwa kwenye majaribu mazito kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo.

“Kikubwa zaidi ni tukio ambalo limetokea katika maisha yangu wiki moja iliyopita, last Thursday,” amesema Q-Chief.

“Nimepata bahati, naweza kusema ni bahati kwasababu watu wengi waliniona kule mtaani wakaniacha. Pengine walikuwa wamelose hope. Lakini nilipigiwa simu na bosi mkubwa tu, anaitwa QS, Joseph Mhonda, Apex Consultants & Associates. Huyu mheshimiwa akaniambiwa kwamba ‘bwana mimi nahitaji kukuona, nahitaji kumuona baba yako tukae tuzungumze kuhusu hatma yako ya muziki. Siamini kama huu ndio mwisho wako, naamini kabisa kwamba wewe ndio msanii wangu bora of all time. Kwahiyo mimi ninayo sababu ya kutaka kukusaidia na wewe una sababu ya kuprove kwamba you are the best’. Kwahiyo tumesaini contract mbele ya baba, mbele ya wanasheria na baada ya kusaini tukaanza process za kurekodi na sasa hivi tuko kwenye mchakato wa kumtambulisha Q-Chief officially kwamba ni wa kampuni ya Qs, yuko under management ya Qs. Tutaita media, tutachoma mbuzi kidogo halafu tutazungumza tuanzie wapi kutoka hapo,” ameongeza.

Q-Chief amesema alikuwa kimya kwa muda mrefu ili kujipa muda kutafakari na kubadilisha muelekeo wa maisha yake.
“Nilikuwa najaribu kujiandaa katika misingi kwamba nimekuwa na ups and downs kwahiyo ilinichukua muda kukaa chini kumuandaa Q-Chief,” anasema msanii huyo.

“Kwahiyo nilisema nikae chini. Nilisema nikae chini, nitulize akili, nijue wapi nimekosea, nani nimemkosea, tunamaliza vipi ili tuanzie hapa. Ni takriban miaka mitano ya maumivu katika maisha yangu na mateso, masimango na manyanyaso, fedheha. Nilichokuja kugundua kuwa kuna watu juu yangu wengine chini yangu ambao tulipishana kauli. Kama mwanadamu naamini kwamba tunakosea lakini tunasemeheana pia.”

“Baba yangu amenipigania sana kipindi nilikuwa kwenye hali ngumu ya kimaisha na wakati mbaya wakati navuta unga. Since then, baba alikuwepo nyumba yangu na ndipo nilipogundua kuwa nina wazazi kumbe sijatupwa tu duniani, sijaokotwa ni mtoto wa mtu fulani tena mtu mkubwa. Ilimuumiza lakini kama baba hakukimbia kumwacha mwanae, alisimama on my behalf kuwa pale kama baba kunionesha upendo, kuniambia ‘mwanangu ulipita njia mbaya, hii ndo njia sahihi. Tukimshirikisha Mungu kila kitu kinawezekana, usifanye vitu peke yako. I am your father you can talk to me. Una wanao, they are looking at you, kesho nitashindwa kuongea nao hawa. It’s good to play you party, don’t be a father, be a daddy, be a sweet daddy. Pengine hukulelewa katika mazingira hayo ambayo unapaswa kuwalea wanao but you can learn through time and situation.’ Kwahiyo ile ilinipa nguvu na msukumo wa kuamka tena na kufanya kitu kizuri,” ameongeza.

“Mashabiki wengi sana walikuwa wanahoji na kuuliza, unajua huwezi kuchukiwa na watu wote, kuna watu ni mashabiki wako die hard wako pale since day one, walikuwa disappointed na walikuwa kwenye maumivu makali sana kama mimi. Walichofanya ni kunishauri na kuongea na mimi kwamba ‘Q-Chief kuna vitu tunavimiss kutoka kwako. Kwahiyo ilinipa nguvu na msukumo kwanza wa kuamsha akili.”

Muimbaji huyo amesema pamoja na kupitia maisha magumu yenye mitihani mingi, amejifunza maisha zaidi na pia yamemjenga kama msanii.

“Nashukuru haya majaribu yamekuja wakati muafaka kwasababu yamejinijenga kwanza kwenye uandishi, kitu ninachoandika sasa hivi kitakugusa tu kwa namna moja ama nyingine. Unaweza kuwaza huyu akili yake imekomaa kiasi gani anaandika vitu vikubwa kama hivi! Lakini wakati nimeanguka nipo chini, huko ndiko palikuwa darasani kwangu mimi. Nilienda kujifunza zaidi kuhusu dunia hii, nikataka niwajue binadamu kwa undani, nikataka kujua nini maana ya uadui, nini maana ya upendo, nini maana ya kusamehe, nini maana ya kusahau na kuanza tena upya.

Q-Chief amedai kuwa pamoja na kutokuwa na uhusiano mzuri na wazazi wenzie, hajutii akikumbuka wale wanayosema juu yake ikiwemo kumdharau.

“Wakati nipo kwenye wakati mzuri hawakuwahi kusema hilo hata siku moja kuwa mimi sio baba au nani, kwasababu mambo yalikuwa yanaenda. And then things turned around and then they started talking. The good thing was, walikuwa wananijenga believe me, I never regretted them talking badly about me. Halafu mimi siwezi kubishana na watoto wa kike ni jinsia mbili tofauti, I am a man, I learn to be strong in life. Hawa ni mama zetu, If we don’t respect what they say you can never get along in what you wanna do. Nilichogundua ni kwamba walipata waume wapya wakakaa chini wakapeana ushauri, I respect that lakini leo nimewahakikisha kwamba kampuni yangu itawasomesha watoto wangu, I will help you from there.”

Q-Chief amewaomba mashabiki wake kumpokea tena kwa moyo mmoja pale atakapotambulisha wimbo wake mpya hivi karibuni.

“Kitu pekee nachotaka kufanya kwenu ni kupata imani yenu kwangu tena kama mlivyoniamini, nawapenda, sina kingine cha kuwaambia.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents