Burudani

Tunda Man adai kuwa na mipango ya kugombea ubunge, japo si 2015

Inaonekana wasanii wengi nchini wanapenda kuingia mjengoni. Baada ya Shilole kutangaza nia ya kugombea ubunge wa Igunda, Tundaman amesema ana nia ya kuja kugombea ubunge wa Kinondoni.
1597244_840582495974190_972969058_n

Akizungumza na Bongo5 Tunda Man amesema ni kweli yupo kwenye mipango hiyo ila sio mapema kutokana kwakuwa bado anahitaji kujiendeleza kielimu zaidi.

“Iddi ni kama baba yangu siwezi gombana naye, ila ninafikiria kufanya kitu kama hicho,” amesema. “Unajua unatakiwa kwanza kuwa mtu wa watu halafu wakupende. Iddi Azan alikuwa mtu wa watu kwenye mechi zetu alikuwa anakuja, ila kwangu mimi bado kidogo inshallah mwenyezi Mungu akijalia nitakuja kufanya hivyo. Kwasababu sasa hivi nina mipango ya kwenda shule tena, inshallah mambo yote yakiwa sawa nitakujafanya hivyo,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents