Michezo

FBI yawatia mbaroni makocha wanne kwa tuhuma za rushwa

Makocha wanne wa chuo kikuu cha mchezo wa Mpira wa Kikapu nchini Marekani ‘NCAA’ wamekamatwa kwa kosa la kuhusika na vitendo vya rushwa.

Serikali ya Marekani imewakamata waalimu hao pamoja na mtendaji mwandamizi kutoka kampuni ya vifaa vya michezo ya Addidas akiwa ni miongoni mwa watu 10 waliyoshikiliwa na kushtakiwa.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliyofanywa na shirika la kipelelezi la FBI’ chini ya Uratibu wa chama cha mchezo wa kikapu pamoja na makocha na wajumbe ambao wamekuwa wakiwapa mafunzo wachezaji wenye vipaji zaidi kuhudhuria mafunzo katika vyuo vingine.

Makocha hao wa ‘NCAA’ waliyokamatwa ni kocha msaidizi wa chuo cha Oklahoma State University, Lamont Evans, kocha msaidizi wa Auburn University, Chuck Person, kocha msaidizi wa University of Arizona, Emanuel “Book” Richardson na Tony Bland  ambaye ni kocha msaidizi wa University of Southern California.

Rais wa Jumuiya ya vyuo vya michezo nchini Marekani  ‘NCAA’, Mark Emmert kupitia maelezo yake hapo jana siku ya Jumanne amesema kuwa  kamwe hawawezi kuvumilia vitendo vya namna hiyo.

“Kamwe hatuwezi kuvumilia tabia ya namna hii, uwalimu ni nafasi nyeti na yakipekee kiasi ambacho unakuwa mwenyekuaminika kwa wanafunzi na familia zao hivyo kama haya madai ya rushwa na upendeleo kwa baadhi ya wanafunzi yatakuwa na ukweli wowote nilazima hatua kali za kisheria na kinidhamu zichukuliwe.” amesema Emmert

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents