Burudani

Fid Q aibariki Sina Muda ya Nay wa Mitego, remix inakuja

Nay wa Mitego amedai kuwa kipindi anaachia wimbo wake ‘Sina Muda’ alipata wasiwasi kama mashairi yake yanaweza kueleweka au yangemweka matatani. Hata hivyo matokeo yamekuwa mazuri ikiwa ni pamoja na Fid Q kuyabariki mashairi yake.

nnnay

Nay ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo umewavuta mashabiki wapya ambao hakutegemea kama wanaweza kumwambia kitu chanya kuhusu muziki wake.

“Sina Muda umeleta kelele nyingi sana mtaani,” amesema Nay. “Watu wangu wa karibu wakainiambia wimbo utafungiwa, nikawa napigiwa simu na watu tofauti tofauti. Lakini nashukuru Mungu matokeo ya wimbo yamekuwa makubwa sana, watu wameelewa. Kutokana na kelele za watu niliingiwa na mashaka huenda ukafungiwa. Lakini umekuwa tofauti hata watu ambao sikuwahi kufikiria kuwa mashabiki wangu, wameupenda,”ameongeza rapper huyo.

“Unajua ni ngumu sana kukutana na msanii mwenzio akakwambia ‘bwana eeh hii ngoma yako sasa hivi nimeipenda kuliko ngoma yako yoyote’, na kwa mara ya kwanza mimi nimekutana na Fid Q akaniambia ‘mdogo wangu wimbo wako wa Sina Muda ndio ngoma katika ngoma zako unazofanya Hip Hop nikaishika, naona ni wimbo mkubwa’, kwahiyo nimekuwa nikikutana na watu wengi wanaonyesha kuukubali sana wimbo,” amesisitiza.

Pia Nay amesema baada ya kupokea maoni ya wasanii mbalimbali kutaka kuurudia wimbo huo, ameamua kufanya nao remix.

“Kiukweli kabisa nafanya remix kwa sababu naweza kuthubutu kusema, kuna wasanii wengi wanatamani wangekuwepo kwenye ule wimbo, nikaona umekuwa wimbo mkubwa na wasanii wengi wanahitaji kuufanyia remix. Kwanini tusifanye remix ya pamoja ili tupate kitu kizuri zaidi? Basi ndo wazo likajengeka na sasa hivi tupo kwenye mipango baadhi ya wasanii waanze kuingiza vocal.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents