Burudani

Fid Q atunukiwa Tuzo ya Heshima

Mkali wa muziki wa hip hop Bongo, Fid Q ametunukiwa tuzo ya heshima.

Tuzo hiyo ni kutokana na kuiwakilisha vyema Kanda ya Ziwa kupitia muziki wake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Jana nimepokea Tuzo ya heshima ya kuwakilisha Vyema kanda ya Ziwa kupitia muziki toka kwa wataalam wa masuala ya mazingira waitwao Kijani Consult Tanzania.

Taasisi, kampuni, wadau n.k wamekuwa wakitambua mchango wa Fid Q katika muziki na uzito wa jina lake. Utakumbuka April 30, 2018 aliteuliwa na Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) kuwa Mwenyekiti wa kamati ya fedha, mipango na uchumi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents