Burudani

Galaxy aeleza sababu ya kumsusia director wa SA video yake mpya

Msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Galaxy amefunguka kwa kuelezea sababu ya kukataa kuikataa video yake mpya aliyoshoot Afrika Kusini na muongozaji wa huko miezi michache iliyopita pamoja na idea ya wimbo wake mpya ‘Top in My Heart’.

galaxy

Akiongea na Bongo5, Muimbaji huyo amedai kuwa sababu iliyomfanya amsusie director video yake aliyoshoot Afrika Kusini ni kutokana haikufikia level ya video aliyokuwa anaitaka.

KUHUSU KUMSUSIA DIRECTOR VIDEO

Sasa hivi nimefanya tena video South Afrika sikuipenda nimeipiga chini, Kwahiyo unaweza ukaona ni vitu gani navitaka, sitaki kitu cha kawaida tu. Ile level niliyokuwa naitaka haikufikia, labda ingekuwa ni kitu kimoja labda ungeweza ungejaribu kumwambia mtu nataka hivi na hivi lakini ni issue kubwa kidogo. Hata nikisema labda narudi yanaweza yakawa ni yale yale kwahiyo najaribu kuangalia utofauti. Wasanii wengi wanakosea sana, wengi sana wanashoot video Afrika Kusini halafu ukiona ni ya kawaida tu, tunatakiwa tuangalie wimbo  wako unahusu nini na unataka nini kwa sababu wasanii wengi wanaenda South Africa wanakimbilia wanaenda kushoot na mameli, magari makali, majumba makali lakini haangalii wimbo wake unazungumzia kitu gani.

AKIONGELEA KUHUSU WIMBO WAKE MPYA ‘TOP IN MY HEART’

Kusema ukweli nilikuwa na msichana wangu mmoja hivi tulikuwa tunapendana sana na mara nyingi nilikuwa naye karibu sana, halafu hili jina nilianzaga kumuita yeye. Nilikuwa nafanya nyimbo na Elly da Bway , mimi na Elly huwa tunashirikiana kila kitu, hii nyimbo tumesaidia na na Elly tumeiandika kila kitu lakini lengo kubwa ni yule msichana alinifanya mimi kupata idea ya ‘Top in My Heart’.

Msanii huyo ameongeza kuwa video ya wimbo huo anaweza akaenda nchini Uganda kushoot video hiyo na director wa huko ambaye alishoot video yake ya kwanza ya Tam Tam, Sasha VYBZ.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents