Burudani

Gelly wa Rhymes: Ninaweza sana kurap, sijawa serious tu

Muimbaji na muigizaji wa filamu, Gelly wa Rhymes amedai kuwa ana kipaji kikubwa cha kurap lakini hajakichukulia serious tu.

Gelly

Gelly ambaye hivi karibuni alitoa version yake ya wimbo Trap Queen ameiambia Bongo5 kuwa kabla ya kuanza kuimba alikuwa akifanya rap.

“Kurap kwa sasa sijakuchukulia serious kwasababu naona market yangu nilishaitengeneza watu wanajua kuwa ninaimba kwahiyo kuwabadilisha inachukua muda,” amesema.

Gelly amesema watu wengi wameshangaza na uwezo wake wa kurap baada ya kusikiliza Trap Queen hivyo anajipanga kutoa cover ya wimbo wa Chris Brown, Ayo.

“Hiyo ndio nitaonesha uwezo wangu wa kuchana sababu nitachana kwa muda mrefu.”

Muimbaji huyo amesema kama ikitokea mtu atakayeweza kusimamia projects zake za nyimbo za rap, anaweza kuingia studio na kufanya wimbo rasmi wa rap.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents