Burudani

Godzilla: Bado nina imani na waongozaji wa video wa Tanzania

Rapper Godzilla aka Zizi amesema bado ana imani kuwa waongozaji wa video wa Tanzania wanaweza kufanya video nzuri kama wasanii wakijiandaa kwa nzuri.

Godzilla2

Amesema anatarajia kumtumia Nick Dizzo kama muongozaji wa video yake wimbo wake mpya ‘You and I’ aliomshirikisha Marco Chali ambaye ameutayarisha pia kupitia MJ Records. “Nick Dizzo ndiye tuliyempendekeza na Marco,” Zizi ameiambia Bongo5. “Kwasababu amefanya video kama za akina Izzo B zimeenda Channel O zinapigwa. Ni kumpa vifaa tu na kukodisha vifaa vya hela nyingi. Bado naamini wabongo wana nafasi nzuri kwasababu ukiangalia watu wanaofanya video nje zinaenda lakini sio zote zinafanikiwa kupita sehemu wanazotaka. Kwahiyo inategemea na upepo wa mtu ameangukaje,” ameongeza.

“Mimi naamini kwenye watu wa ndani sana, mimi naamini watu wana vitu vingi. Kuna mambo tu Bongo yanatukwamisha labda kwa system ama vitu fulani lakini watu wana uwezo mkubwa sana Tanzania.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents