Burudani

Producer Nahreel akiri beat za ladha ya Kiafrika zimempa ‘neema’ zaidi

Producer wa Home Town Records, Nahreel ambaye mwaka huu ametajwa kuwania kipengele cha mtayarishaji bora wa muziki – kizazi kipya kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro, amesema tangu aanze kutengeneza nyimbo zenye midundo ya Kiafrika maarufu kama ‘Afro Pop’ amekuwa akitafutwa zaidi na wasanii kuliko ilivyokuwa mwanzo ambapo alikuwa akijulikana kama producer wa hip hop.

Nahreel

Akiongea na Bongo5, producer huyo ambaye ametengeneza hits zikiwemo ‘Nje ya Box’ ya Weusi, Chelewa ya Navy Kenzo, Come Over ya Vanessa Mdee na zingine, amesema pamoja na kujulikana zaidi mwaka jana kwa nyimbo za aina iyo, uwezo wa kuzitengeneza anao tangu siku nyingi japo alikuwa anapendelea zaidi kutengeneza muziki wa hip hop.

“Nilipoamua kuweka nguvu nyingi kwenye hizi beat za afro pop niliamua kuja na kitu tofauti na kama ulivyosikia Chelewa na Come Over niliamua kuweka identify fulani ambayo mtu akisikia hiyo beat atajua huu ni mkono wa Nahreel,” amesema.

“Ni kweli changes zilizotokea ni kubwa na tangia nianze kutengeneza hizo beats wasanii wengi wamekuwa wakija pale studio pale Home Town wakitaka niwatengenezee beats za aina hiyo. Kwahiyo changes ni kubwa kupita hapo nilipokuwa natengeneza beats za hip hop,” ameongeza Nahreel ambaye pia ni member wa kundi la Navy Kenzo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents