Michezo

GSM atoa Mil 100 kila bao kwa Yanga

Picha iko hivi; Yanga wamewaahidi mastaa wao Sh 100Mil kila bao watakalofunga dhidi ya Mamelodi. Kumbuka, Simba na Yanga mpaka sasa zina uhakika wa Sh 2.3Bil kama zawadi kwa kucheza hatua ya robo fainali lakini yoyote atakayefuzu nusu tu mkwanja unaongezeka kufikia Sh 3Bil kwahiyo hata wakichomoa kwenye hiyo bado klabu zitabaki na cha juu.

Yanga wakati wanacheza mechi yao ya kwanza nyumbani dhidi ya Mamelodi Sundowns vigogo wao waliwawekea mezani kiasi cha Sh 300Mil endapo itafanikiwa kushinda matajiri hao wa madini lakini mechi hiyo ikamalizika kwa suluhu.

.Kuhakikisha matokeo ya sare yoyote ya mabao au ushindi yanayohitajika na Yanga ili ifuzu nusu fainali yanapatikana kwenye mchezo wa ugenini utakaopigwa Ijumaa saa 3:00 usiku, Kigogo wa Yanga, GSM ameongeza dau zaidi akiwaambia mastaa wao kuwa kila bao la mchezo huo litakuwa na thamani ya Sh 100Mil.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents