Habari

Hakimu akubali hoja moja kati ya mapingamizi matatu kesi ya Sabaya

Mahakama ya Hakimu Mkazi, Arusha leo imekubaliana na pingamizi moja kati ya matatu yaliyowekwa na upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake Sita.

Sabaya akiteta jambo na Wakili wake Mosses Mahuna mahakamani

 

Akisoma uamuzi mdogo Hakimu Mwandamizi, Dk. Patricia Kisinda amesema mahakama imekubaliana na hoja moja kuhusu nakala ya leseni ya udereva iliyopo kwenye ‘mandate file’ ndiyo haikufata taratibu za kisheria.

Aidha katika hatua nyingine mahakama imetupilia mbali pingamizi la utetezi la kutaka mahakama isipokee ushahidi wa nyaraka ambazo ni Bank Statement, Bank Slip na nyaraka zingineze kwa kuwa hazina mashiko kisheria kutumika kama kielelezo cha ushahidi.

Wakati akitoa ushahidi siku ya jana Nov 16, Shahidi w Jamhuri, ambaye ni Meneja wa CRDB Tawi la kwa Mromboo, Jijini Arusha Ndg. Marry Kimasa aliiomba mahakama ipokee nyaraka hizo na zitumike kama ushahidi.

Dk. Kisinda amesema kwamba, mahakama imeona kwamba nyaraka zingine zilizotolewa na shahidi zina mashiko kisheria kupitia kifungu cha 78, 79.

Kesi ya Uhujumu uchumi bado inaendelea ambapo Shahidi anaendelea kutoa ushadi wake namna ambavyo mteja wake Francis Evarist Mrosso alivyotoa Milioni 90 siku ya Januari 22, 2021 kwenye tawi la kwa Mromboo.

BY: Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents