Michezo

Hali ya Neymar bado tata, Kurudishwa kwao Brazili

Klabu ya Paris Saint-Germain imefikia maamuzi ya kumpeleka nyota wa timu hiyo, Neymar Jr nchini Brazili kwaajili ya upasuaji wa kifundo chake cha mguu kufuatia kuumia katika mchezo waliyochomoza na ushindi wa 3 – 0 dhidi ya Marseille.

Neymar mwenye umri wa miaka 26, atasafirishwa hadi Brazili wiki hii kwaajili ya matibabu huku madaktari kutoka ndani ya klabu ya PSG na timu yake ya taifa ya Brazili wakishirikiana pamoja kuhakikisha mshambuliaji huyo ghali zaidi duniani anarejea katika hali yake ya kawaida.

Taarifa iliyothibitishwa na klabu ya Paris Saint-Germain ya nchini Ufaransa hapo jana siku ya Jumatano ni kuwa mshambuliaji huyo ataukosa mchezo wa marudiano wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi Real Madrid.

Baada ya matibabu ya siku tatu yaliyo waunganisha madaktari wa pande zote mbili klabu ya Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Brazil mchezaji mwenyewe Neymar Jr amependekeza kutibiwa nchini kwao mwishoni mwa wiki hii.

Atakuwa chini ya Dr. Rodrigo Lasmar kwa upande wa Brazili na Profesa Saillant atakayeiwakilisha PSG.

Meneja wa PSG, Unai Emery hapo hawali alisema kuna uwezekano mdogo kwa Neymar kuwepo katika mchezo ujao wa klabu bingwa siku ya Jumanne dhidi  ya Real Madrid.

PSG, itakosa huduma ya Neymar  dhidi ya mwenye jumla ya mabao 19  na pasi 13 zilizochangia mabao msimu huu Ligue 1.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents