Michezo
Hamisi Kiiza aibukia klabu ya Free state Stars ya Afrika Kusini
Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga, Hamisi Kiiza ameasajiliwa na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini inayaoshiriki ligi kuu.
Kiiza baada ya kutemwa na klabu ya Simba aliyodumu nayo kwa msimu mmoja tu, Kiiza amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili akiwa chini ya kocha wa klabu hiyo Rantsi Mokoena.
Hamisi Kiiza atambulishwa rasmi pamoja na wachezaji wengine walio sajiliwa na klabu hiyo ya Free State Stars ya Afrika Kusini.