Michezo

Haondoki mtu: Tshabalala kusaini mkataba wa miaka miwili na Simba

Hatimaye beki wa klabu ya Simba FC, Mohamed ‘Tshabalala’ Hussein anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na kuanza kupunguza presha za mashabiki wa timu hiyo waliofikiria kuwa anaondoka.

14368931_694800517342380_1686475417_n

Akiongea na Dar 24, Meneja wa mchezaji huyo, Herry Mzozo amesema, “Ninaweza kusema Tshabalala amebakisha kama asilimi 20, kukamilisha taratibu zote za kuendelea kuitumikia simba, labda nikuweke wazi kinachoendelea hivi sasa ni masuala ya kibenki ambayo yatakamilisha huu mchakato.”

“Viongozi wa Simba walikua na mazungumzo ya muda mrefu na Tshabalala na nikueleze kwamba, hatua hii ilianza tangu mwanzoni mwa msimu huu na ukaribu uliopo baina ya mchezaji wangu na uongozi wake ndio umekuwa chachu ya mafanikio ya kusainiwa kwa mkataba wa miaka miwili,” ameongeza.

“Ninaweza kusema katika suala hili Yanga walizushiwa, lakini hakuna ukweli wowote kuhusu mipango iliyokua ikiendelea chini chini kumuhusu Tshabalala, japo kwa upande wangu ninazichukulia taarifa hizo kama kunogesha mchezo wa soka ambao siku zote umekua na maneno mengi.”

Awali mchezaji huyo alidaiwa kuwindwa kwa karibu na timu ya Yanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents