Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

Harmonize anunua mashamba ya miwa? aongea haya

Msanii wa muziki wa bongo Fleva Harmonize ameonekana kwenye mashamba ya miwa huku akiwaasa wasanii wenzake kuwa wawekeze shambani maana ndio pesa ilipo.

Kupitia clip fupi ya video aliyoipost Insta stori ameeleza kuwa kuna maisha baada ya kutumia pesa zako club, pesa ipo shambani.

Mbali na hilo Harmonize ameonekana akiendesha trekta la miwa huku akipakia miwa hiyo kwenye magari ya kubebea miwa, haijajulikana Harmonize yupi kwenye mashamba yapi Tanzania na ni kweli ameenda kuwekeza shambani au ameenda ku-shoot video ya muziki.

Related Articles

Back to top button