Burudani

Hatimaye Izzo Bizness amjibu Rayvanny (+video)

Rapper Izzo Bizness amesema si kweli kwamba anafanya muziki wake bila msongo wa mawazo (stress) kama alivyodai Rayvanny.

Katika ngoma ya Rayvanny ‘Tabia’ alidai kati ya wasanii wasio na stress na muziki wa Bongo ni Izzo Bizness na Quick Rocker.

Izzo Bizness amesema Rayvanny atakuwa ametazama katika mtazamo wake lakini huu muziki ni biashara kama vilivyo biashara nyingine na ups and down zinakuwepo.

“Stress zinakuwepo sisi kama binadamu hii ni biashara kuna kipindi unaweza usijisikie vizuri unatoa wimbo usipokelewe kama ulivyokuwa umetarajia,” amesema Izzo.

“Kikubwa ni nidhamu, kuishi vizuri na watu na kujitahidi kutengeneza muziki mzuri kwa sababu hata kama unakuwa haupo namba moja si kwamba haustahili kuwa nambo moja, kusema tunafanya bila stress sio kweli,” ameongeza.

Izzo Bizness kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina Saa Sita.

Soma zaidi Alikiba, Diamond, Nay, Dimpoz, Young Dee, Shilole, Joh Makini wachanwa na Rayvanny

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents