Michezo

Haya ndio maamuzi ya kamati ya saa 72 kwa katibu mkuu wa Rhino Rangers

Kamati ya usimamizi na uendeshaji imempa adhabu ya Kumfungiwa miezi mitatu Katibu Mkuu wa Rhino Rangers, Dickson Cyprian Mgalike kwa kosa la kuidanganya kamati kwa kutoa taarifa potofu katika barua aliyoiandikia Bodi ya Ligi.

tff-1

Hapo awali, Kamati ilimuadhibu Mchezaji Sameer Mwinyishere kwa kosa la kumrushia chupa ya maji mwamuzi.

Katibu aliandika barua kusema kwamba Sameer hakufanya kosa hilo na alimtaja mchezaji Yusuf Mputa kwamba ndiye aliyefanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kumrushia Mwamuzi chupa ya maji.

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji kwa kushirikiana watendaji wa Bodi ya Ligi ilifanya uchunguzi na kubaini mchezaji Yusuph Mputa hakuwepo kwenye Orodha ya Wachezaji wa siku hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kufuata kanuni ya 41(6).

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents