Burudani

Mtoto mwenye jinsia mbili akubaliwa na mahakama kuondoa ya kiume

Mtoto wa miaka mitano raia wa Australia aliyezaliwa huntha; akiwa na sehemu za siri za kike na kiume amekubaliwa na makahama kubadilisha jinsia yake na kuwa mwanamke japo hatakuwa na uwezo wa kuzaa.
_92865069_48b00ed7-7bec-41f3-8b38-3c9fe64df8cb

Mtoto huyo anayejulikana kwa jina moja tu la Carla anajitambulisha kama msichana japo hana viungo sawa vya kike. Mahakama imeitikia ombi la wazazi wake kufanyiwa upasuaji wa kuondoa sehemu za siri za kiume.

Wazazi wa Carla wamesema walitaka kujua kama ni sawa kuamua mwana wao afanyiwe upasuaji wa kubadilisha jinsia yake na kuwa mwanamke, lakini baada ya upasuaji hali yake haitaweza kurekebishwa tena ikiwa mtoto huyo atabadilisha mawazo akiwa mtu mzima na kutaka kurejea mwanamme.

Mahakama ya masuala ya familia iliambiwa Carla alizaliwa akiwa na baadhi ya sehemu za kike na akawa na tabia za kike, kupenda vichezea vya watoto wasichana, nguo za kike na michezo ya waoto wasichana. Wataalamu wa afya wamesema upasuaji huo utasaidia Carla kuotokua na hatari ya kupata saratani japo hataweza kutunga mimba.

Upasuaji huo unastahili kufanyiwa kabla ya mtoto huyo kufikia miaka ya kuvunja ungo. Mahakama hiyo ilisema wazazi wanaweza kumsaidia mwana wao kufanyiwa upasuaji bila idhini yeyote.

Baadhi ya wanaharakati wa haki za watu huntha wamelalamikia hatua ya mahakama na wazazi wakisema ilifaa mtoto kuyo kujiamulia wakati akiwa mtu mzima.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents