Burudani

Huddah awachana wasanii wa Kenya kuhusu sakata la Play Kenya Music

Mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe amefunguka mtazamo wake wa kwanini? anapenda sana kusikiliza nyimbo za wasanii wa Nigeria kuliko Kenya.

Related image

Huddah kupitia Instagram Stories, amesema kuwa muziki wa Nigeria unahusisha maisha halisi ya kwenye jamii. Huku akiuponda muziki wa Kenya ambao amedai kuwa nyimbo nyingi ni za mapenzi, zina sifia ulevi na madawa ya kulevya .

Unajua kwanini huwa huwa nasikilisa sana muziki wa Nigeria? unaniingia sana moyoni, kwa sababu nasikiliza kile kitu nataka kusikiliza, wenzetu wameamka sana. Ujumbe uliopo kwenye nyimbo zao sio tu mapenzi na madawa ya kulevya, bali wanazungumzia maisha halisia. Kiukweli wananivutia, na hivyo ndio vitu tunataka kusikia. Na sio kila siku kuimbia ngono, mapenzi na madawa ya kulevya,” ameandika Huddah .

Kwa upande mwingine Huddah amewapongeza wasanii kama Nyashinski, Sauti Sol, Octopizzo na Khaligraph Jones kwa kufanya muziki mzuri na kuitangaza Kenya kimataifa .

Kwa sasa nchini Kenya kuna kampeni ya PLAY KENYA MUSIC inayoshinikiza Radio&TV nchini humo kucheza muziki wa ndani kwa asilimia kubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents