Habari

Hujachelewa kufanya mabadiliko ya maisha yako

Watu wengi hupenda kulaumu maisha waliyopitia au wazazi waliowakuza na kuendelea kuishi huku wakirusha lawama kedekede kwa wale ambao waliwalea au kuwakuza.

pensive woman biting lips

Wiki hii nimekutana na mtu wa tofauti kidogo ambaye amenifanya kuandika makala hii kwamba hujachelewa kufanya mabadiliko ya maisha yako kwakuwa historia yako haiwezi kubadilisha maisha yako ya mbele ila maamuzi utakayofanya sasa yatabadilisha maisha yako yanayokuja.

Na si huyu peke yake bali hata kuna wengine wengi ambao wamepitia maisha fulani ambayo kwa namna moja ama nyingine inakuwa sababu ya kutokuendelea na kubaki na lawama nyingi.

Watu hawa wachache ambao hawakusoma shule nzuri kama wewe na mara nyingine hawakupata fursa ya kuendelea na masomo kutokana na ukosefu wa ada na maisha magumu lakini leo wanaongelea habari tofauti kabisa. Wanapoongea utagundua kitu tofauti na watu wengine ni kwamba walifika sehemu hawakuridhika na kile walichonacho wakaamua kufanya maamuzi ya kujiendeleza katika utu uzima wao na sasa hawapo kama walivyokuwa.

Historia yako ni ya kwako wala haiwezi kubadilika, ila maisha yako ya baadaye yanaweza kubadilishwa ukiamua. 

Hili ni jambo ambalo watanzania wengi ni wazuri wa kulalamika na kulaumu waliopita, ukilaumu itakusaidia nini? Hakuna. Kitu ambacho unaweza kufanya ni kuamua kubadilika kwa namna unavyofikiri na unavyofanya maamuzi. Mfano kama ulikosa elimu ya chuo uliishia elimu ya sekondari, umechukua maamuzi gani ya kutafuta fursa zilizopo ukaweza kujiendeleza ili ufikie malengo yako ya kuwa na elimu ya juu? Utasingizia vitu vingi sana ila ukweli wa mambo ni kwamba hujaamua kufanya maamuzi magumu ili uweze kutoka hapo ulipo.

Ukisikiliza watu hao ambao walipaswa kuwa na lawama kama watu wengine walichagua ni kwamba lawama hazisaidii ila maamuzi utakayoamua sasa yatabadilisha maisha yako ya baadaye.

Suala ni kwamba unafikiriaje maisha yako ya baadaye na kitu gani unataka kufanya sasa ili kubadilisha maisha yako ya baadaye?

Hakuna msaada ambao mtu atakupa kama wewe mwenyewe hujaamua kufanya mabadiliko. Watu wengi tunapenda mabadiliko lakini hatutaki kubadilika na tunategemea mabadiliko yatakuja. Napenda kukufahamisha kuwa hiyo itakuwa ndoto mpaka unaingia kaburini, ila ukiamua kubadilisha mtizamo wako wa mambo kuna vitu vingi vitabadilika kwenye maisha yako. Hujachelewa kuanza kitu kipya kwa mtizamo mpya, maisha yako ya baadaye yanategema maamuzi unayofanya sasa.

Je ni vitu gani ambavyo havikuwezekana miaka iliyopita lakini sasa vinawezekana?

Unatakiwa kujiuliza, ninatakiwa kuadilika wapi na katika mtizamo gani? ninataka kuishi maisha gani au kuwa naujuzi gani? nifanyeje? Je Kuna njia mbadala? Ukishindwa kufikiri omba msaada utasaidia kujua vitu ambavyo hujaweza kuvijua. Fikiri kabla ya kutenda.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents