Habari

Hutaamini dola moja ni sawa na shilingi ngapi ya Tanzania kwa sasa! Wachumi wakuna vichwa (Video)

Unataka kwenda kuchenji fedha ili kupata dola ya Marekani? Jiandae kisaikolojia kwakuwa unaenda kukutana na mshtuko wa haja!

Dola moja ya Marekani sasa inabadilishwa kwa shilingi 2010 hadi 2050 kwenye maduka ya kubadilishia fedha za kigeni! Hilo ni anguko la shilingi ya Tanzania la zaidi ya asilimia 20 katika kipindi cha mwezi mmoja peke yake.

Kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania kunaashiria kuwa uchumi wa nchi unazidi kuporomoka kwa kasi!

Chanzo chake ni nini? Mwenyekiti wa taifa wa NCCR – Mageuzi, James Mbatia ambaye pia ni waziri kivuli wa fedha anataja matumizi ya fedha za kigeni nchini kama chanzo kikubwa cha poromoko hilo.

“Badala ya kujitambulisha kama taifa letu, kwa kutumia shilingi yetu tunatumia fedha za kigeni na hasa dola ya Marekani,” Mbatia aliwaambia waandishi wa habari Jumatano hii.

“Na unapopangilia uchumi wako kwa kutumia dola ni kwamba huku hujaangalia mambo mengine kwa mfano mauzo yako nje zaidi ya manunuzi yako nje, matumizi yako yanayohitaji fedha za kigeni, uchumi wako utayumba kweli kweli. Mauzo yetu ya nje ni kidogo sana ukilinganisha na tunavyohitaji kununua kutoka nje.”

Mbatia aliitaka benki kuu ya Tanzania ifanye kila jitihada kuhakikisha kuwa thamani ya shilingi ya Tanzania inapanda tena.

“Tuitake benki kuu isiendelea kukaa kimya, tuitake serikali isiendelee kukaa kimya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents