Ice Bucket Challenge: Huyu ni msanii wa Kenya aliyetupa karata yake (Video)

Kampeni ya Ice Bucket Challenge, ambayo wakati mwingine huitwa ALS Ice Bucket Challenge, huhusisha kujimwagia maji yenye barafu ili kukuza uelewa kuhusiana na ugonjwa uitwao ‘amyotrophic lateral sclerosis’ (ALS) na kusisitiza umuhimu wa kuchangia fedha kwaajili ya utafiti.

DSC_0004-copy
Sheikha

Matukio hayo yamekuwa maarufu sana kwenye mitandao ya kijamii siku za hivi karibuni ambapo mastaa kibao dunia wameshiriki. Challenge hiyo huanza kwa mtu kumtaja mwingine kushiriki ambapo anatakiwa kuchukuliwa video akimwagiwa maji kichwani nao kuwataja wengine kufanya hivyo ndani ya saa 24.

Muimbaji wa muziki wa Kenya aishie nchini Qatar, Mercy Wangare aka Sheikha amekuwa msanii wa kwanza kutoka Kenya kufanya hivyo. Mtazame.

Related Articles

Back to top button