Ifahamu programu ya kijasusi inayouzwa kwa serikali kudukua mawasiliano (+ Video)

Wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi wa habari na mawakili kote ulimwenguni wamelengwa na programu hasidi ya simu iliyouzwa kwa serikali za kiimla na kampuni moja ya Israeli ili kuwadukua mawasiliano yao.

Watu hao wako kwenye orodha ya nambari za simu 50,000 za watu wanaofuatiliwa na wateja wa kampuni hiyo, kutokana na ripoti ya NSO Group, iliyovuja kwa vyombo vya habari. Haikubainika orodha hiyo ilitoka wapi – au ni simu ngapi zilikuwa zimedukuliwa.

Ripoti inaendelea kusema programu hiyo imekusudiwa kutumiwa dhidi ya wahalifu na magaidi na inapatikana tu kwa wanajeshi, watekelezaji wa sheria na mashirika ya ujasusi kutoka nchi zilizo na rekodi nzuri za haki za binadamu.

Ilisema uchunguzi wa mwanzo ambao ulisababisha ripoti hizo, na Shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake mjini Paris la Forbidden Stories na shirika la haki za binadamu la Amnesty International, “ulikuwa umejaa habari potofu na nadharia ambazo hazina uthibitisho”.

Madai juu ya utumiaji wa programu hiyo, inayojulikana kama Pegasus, yalichapishwa Jumapili na Washington Post, Guardian, Le Monde na mashirika mengine 14 ya vyombo vya habari ulimwenguni.

Pegasus huweza kuzidukua simu za iPhones na vifaa vya Android na kupakua jumbe, picha na barua pepe, kurekodi simu na kuwasha maikrofoni na kamera kwa siri.

Nambari zilizo kwenye orodha hazikutolewa, lakini vyombo vya habari vinavyofanya uchunguzi kuhusu madai hayo vilisema wamegundua zaidi ya watu 1,000 katika nchi 50.

Miongoni mwao ni wanasiasa na marais wa nchi, maafisa wakuu watendaji wa biashara, wanaharakati, na wanafamilia kadhaa wa falme za Kiarabu. Zaidi ya waandishi wa habari 180 pia walipatikana kwenye orodha hiyo, kutoka kwa mashirika yakiwemo CNN, New York Times na Al Jazeera.

Nambari nyingi zilikusanywa katika nchi 10: Azerbaijan, Bahrain, Hungary, India, Kazakhstan, Mexico, Morocco, Rwanda, Saudi Arabia na Falme za Kiarabu, kulingana na ripoti hizo.

Walipoulizwa maswali na mashirika yaliyohusika katika uchunguzi, wasemaji wa nchi hizi walikana kwamba Pegasus ilitumiwa kukanusha kwamba walitumia vibaya nguvu zao za ufuatiliaji.

Haikufahamika ni simu ngapi kwenye orodha hiyo zilikuwa zimelengwa, lakini uchambuzi wa kina wa simu 37 ulionyesha kulikuwa na “jaribio na mafanikio”, Washington Post iliripoti.

Hii ni pamoja na watu wa karibu na mwanahabari wa Saudia Jamal Khashoggi, ambaye aliuawa wakati akitembelea ubalozi mdogo wa Saudi Arabia huko Istanbul, Uturuki, mnamo Oktoba 2018 na mwili wake kukatwakatwa

Uchunguzi uligundua kuwa programu za ujasusi ziliwekwa kwenye simu ya mchumba wake siku chache baada ya mauaji yake, na kwamba simu ya mkewe ililengwa na programu kama hizo kati ya Septemba 2017 na Aprili 2018.

Kikundi cha NSO kilisema teknolojia yake “haikuhusishwa kwa njia yoyote na mauaji “.

Simu ya mwandishi wa habari wa Mexico Cecilio Pineda Birto pia ilionekana mara mbili kwenye orodha, pamoja na mwezi mmoja kabla ya kuuawa, uchunguzi uligundua.

Simu yake ilitoweka kutoka eneo la mauaji kwa hivyo uchunguzi haukuwezekana, lakini NSO ilisema kwamba hata ikiwa simu yake ililengwa, hiyo haikumaanisha kuwa data iliyokusanywa ilihusishwa na mauaji yake.

Maelezo zaidi juu ya nani amelengwa yanatarajiwa kutolewa katika siku zijazo.

NSO

WhatsApp ilishtaki NSO mnamo 2019, ikidai kampuni hiyo ilisababisha mashambulio ya kimtandao kwa simu za rununu 1,400 zinazohusu Pegasus. Wakati huo, NSO ilikana makosa yoyote, lakini kampuni hiyo imepigwa marufuku kutumia WhatsApp.

Madai hapa sio mapya lakini kilicho kipya ni kiwango cha kulenga watu wasio na hatia. Karibu waandishi 200 kutoka nchi 21 wana nambari zao za simu kwenye orodha hii na majina zaidi ya watu mashuhuri wa yatafichuliwa .

Kuna mengi ambayo hayajulikani katika madai haya – pamoja na orodha hiyo inatoka wapi na ni nambari ngapi za simu zilizolengwa kikamilifu na programu hiyo. Kundi la NSO kwa mara nyingine limejitokeza kukana mashtaka yote lakini ni pigo kwa kampuni inayojaribu kurekebisha sifa zake.

Wiki mbili tu zilizopita walitoa “ripoti ya uwazi” ya kwanza inayoelezea sera na ahadi za haki za binadamu. Amnesty International ilipuuza ripoti hiyo yenye kurasa 32 kama “Hati ya kuboresha mauzo”.

Madai haya ya hivi karibuni yataharibu sifa zake hata zaidi, lakini hayataumiza kampuni hiyo kifedha. Kuna kampuni chache sana za kibinafsi zinazoweza kutoa aina ya zana za kupeleleza ambazo NSO inauza, na kwa sasa soko lisilodhibitiwa la progamu kama hizo limeshamiri.

Bofya hapa chini kufuatilia.

https://www.instagram.com/p/CRinvmQDsSe/

Related Articles

Back to top button