Michezo

Isco akubali yaishe Real Madrid, mbishi Zlatana kutua Italia na Barcelona yakana kutoa euro mil 15 kwa Griezmann

Tottenham wanampango wa kumnunua kiungo wa kati wa Uhispania wa miaka 21 Carles Alena kutoka Barcelona mwezi Januari. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Image result for carles alena

Manchester United huenda ikaongeza juhudi ya kumsajili Mario Mandzukic 30, baada ya mshambuliaji wa Juventus na Croatia kupunguza masharti ya marupu rupu yake. (Sun)Mario Mandzukic

Mario Mandzukic

Real Madrid imemwambia kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City Brahim Diaz, 20, kwamba inataka kumuuza. (Mail)

 

Mchezaji wa safu ya kati ya Real Isco, 27, amekubali kuwa mmoja wa wachezaji watakaoondoka klabu hiyo mwezi January mwakani. (Mail)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Paris St-Germain na Juventus, Zlatan Ibrahimovic,38, anataka kurejea katika ligi kuu ya Italia, Serie A.Zlatan Ibrahimovic

Zlatan Ibrahimovic(katikati)

Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa zamani wa Uswisi katika klabu ya LA Galaxy unakamilika mwisho wa mwaka huu. (CalcioMercato)

Barcelona imepinga madai kuwa imeilipa Atletico Madrid euro milioni 15 kumaliza mzozo kati yake na klabu hiyo kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28. (Sport)

Juventus na Atletico Madrid ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia beki wa West Brom Nathan Ferguson, 19. (Sun)Nathan FergusonBeki wa West Brom, Nathan Ferguson

Meneja wa chuo cha mafunzo ya soka ya Manchester United Nicky Butt anasema klabu hiyo inawachezaji wengi ambao wanaweza kufuata nyayo za mshambuliaji Marcus Rashford na kuleta mabadiliko katika kikosi cha kwanza. (Goal)

Crystal Palace itamenyana na Aston Villa katika juhudi za kumsajili mshambuliaji wa Colombia Alfredo Morelos, 23, kutoka Rangers mwezi Januari. (Express)Alfredo MorelosMshambuliaji wa Colombia, Alfredo Morelos

Kocha wa zamani wa Tottenham Glenn Hoddle anadai kuna wachezaji “wanne au watano” katika kikosi cha Mauricio Pochettino ambao wanajua wataondoka katika klabu hiyo mwanzo wa msimu ujao. (Express)

Beki wa zamani wa Manchester United Jaap Stam ambaye anatarajiwa kujiunga na Feyenoord msimu huu wa joto anasema kuwa alikataa nafasi aliyopewa ya kuwa meneja wa Newcastle. (Voetbal International – in Dutch)Jaap StamJaap Stam

Newcastle imepinga madai hayo na kusisitiza kuwa haijawahi kuwa na mpango wa kumuajiri mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi. (Chronicle)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents