Habari

Islamic State wadai kuhusika kwenye shambulio la London

Jeshi la polisi nchini Uingereza wamekuwa wakifanya msako kwenye makazi manne mjini London hadi usiku wa manane kama sehemu ya uchunguzi juu ya shambulio la Jumamosi ambapo watu saba waliuawa na wengine wapatao hamsini walijeruhiwa .

Wachunguzi wanajaribu kubaini ikiwa wanaume watatu walioendesha basi lao dogo na kuwagonga wapita njia kabla ya kuwachoma visu wengine wengi walipata msaada wowote.

Kundi la Islamic State limesema lilihusika na shambulio hilo.

Watu kumi na mmoja wanashikiliwa kufuatia uvamizi wa polisi mashariki mwa London.

Mwanamke mmoja raia wa Canada aliyeuawa katika shambulio la London ametajwa katika vyombo vya habari.

Taarifa ya familia yake imesema kuwa alikuwa akifanya kazi katika hifadhi ya wasio kuwa na makazi kabla ya kuhamia Ulaya kuishi na mchumba wake.

Watu 21 waliojeruhiwa katika shambulio hilo wako katika hali mahututi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents