Burudani

Harmonize adai Rich Mavoko tayari kasaini label ya ‘ WCB ‘ ya Diamond

Mmoja kati ya member wa ‘label’ ya WCB, Harmonize amedai kuwa Rich Mavoko ni mmoja kati ya wasanii wa label hiyo.
Diamond na Rich Mavoko

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatano hii, Harmonize alisema label ya WCB ina wasanii watatu yeye mwenyewe , Raymond aliyekuwa Tip Top Connection pamoja na Rich Mavoko.

“Unajua mwanzo zilikuwa ni tetesi lakini naweza kusema ‘its official’ sasa Rich Mavoko yupo chini ya WCB,” alisema Harmonize

Aliongoza, “Kusema kuwa Rich Mavoko amenyoosha mikono kwa Diamond si vizuri kwani watu wanaweza kupata picha tofauti maana si unajua watu wanaweza kupokea jambo kwa maana na ikaleta picha mbaya wakati ni jambo la kawaida,”

Hata hivyo Bongo5 imejaribu kumtafuta Rich Mavoko bila mafanikio, kwani kila akipigiwa simu hapokei wala hajibu meseji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents