Habari

Unataka kampuni yako ifanikiwe? Je wafanyakazi wamezeshwa?

Je wafanyakazi wako wamewezeshwa kwa kiasi gani? Je ni vigezo gani vinaweza kutumika kuwawezesha wafanyakazi wako? Hebu tutizame mambo ambayo yanaweza kukusaidia kuwawezesha wafanyakazi wako.

boss

1. Wajulishe mipango yako

Wafanyakazi wengi hufanya vizuri zaidi pale wanapojua mambo ya kile wanachokifanya au wanachokifanyia kazi kwa kujua ni nini malengo  na matarajio yake. Kama mwajiri wape sura nzima ya kile ambacho wanatakiwa wakamilishe hivyo watafanya bila kusimamiwa na wewe.

2. Usiwatupie lawama watu wengine

Unapowatupia watu lawama hutapata majibu unayoyahitaji. Badala ya kuwanyoshea vidole tafuta tatizo liko wapi kwenye mfumo unaotumia harafu rekebisha hapo, inawezekana kuna kitu kinatakiwa kubadilika ili mambo yafanyike vizuri.

3. Uwe Msikivu

Hiki ndio kitu mabosi wengi hujisahau. Hupenda kusikia wafanyakazi wanasema nini ila hawasikilizi wanachosema wafanyakazi wao. Kusikiliza ni kufanyia kazi mile ulichosikia, na wafanyakazi hupenda pale wao pia wanaposikilizwa kwani halo huongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi. Kumbuka utu kidogo unakupeleka mbali zaidi.

4. Wathamini wafanyakazi wako

Hapa ni katika lugha unayotumia kuzungumza nao, unavyowatazama hiyo huonyesha kwa kiasi gani una wathamini. Onyesha kwa matendo namna unavyo wathamini itaongeza uaminifu wao kwako.

5. Wapongeze na kuwatambua

Unapowapuuza na kutotambua mchango wao usitegemee kupata matokeo yale yale katika kazi. Weka malengo ambayo wanatakiwa wayafikie na vile vile wapongeze waziwazi wanapofanya vizuri. Hiki kitawafanya wawe na malengo ya muda mrefu katika kampuni au shirika lako.

Kuwawezesha wafanya kazi wako ni sawasawa na kuwezesha kampuni au shirika lako. Wanapohamasishwa hawatashindwa kwenda mwendo wa ziada kiutendaji hivyo kufanya kampuni yako kufanikiwa zaidi.

 

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents