Habari

Jeshi la Polisi nchini lashirikiana na Rwanda kutafuta mwarubaini wa uhalifu mitandaoni

Leo tarehe 4 Desemba 2017, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amekutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Rwanda, Emanuel Casana kutathmini makubaliano yaliyofikiwa  mwaka 2012 kuhusu ushirikiano na kufanya oparesheni za pamoja kukabiliana na uhalifu mitandaoni .

IGP Sirro amesema walisaini makubaliano ya kufanya operesheni kwa pamoja na Rwanda ili kukomesha uhalifu mitandaoni na kubadilishana wataalamu.

Wenzetu wa Rwanda ni wazuri kwenye masuala ya kudhibiti uhalifu wa kimtandao, hivyo watatoa mafunzo kwa wataalamu wetu.” amesema IGP Sirro.

Sirro amesema tayari kuna wataalamu kutoka Rwanda ambao watatoa mafunzo ya kushughulikia makosa ya kimtandao.

Akielezea mafanikio waliyoyapata tangu wasaini makubaliano hayo,  IGP Sirro amesema wamepata mafanikio ya kukamata dawa za kulevya zikiwemo bangi mkoani Kagera na kuimarisha usalama katika ukanda huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents