Burudani

Joh Makini aeleza kwanini alimtumia producer wa Kenya R-Kay kwenye ‘Perfect Combo’

Joh Makini si rapper anayezoeleka kirahisi.

Mara nyingi nyimbo zake zimekuwa zikija na ladha tofauti tofauti huku wimbo wake wa sasa, Perfect Combo aliomshirikisha msanii wa Nigeria, Chidinma ukiwa na ladha ya rhumba.

Ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo ulizaliwa Nairobi alipoenda kwenye show ya Coke Studio.

Anadai kwakuwa alikuwa akitaka kutengeneza muziki tofauti, alimfikiria R-Kay mapema kutokana na kufahamika kwa kutengeneza muziki wenye utofauti mkubwa.

Ameongeza kuwa alipoenda kwenye studio zake, producer huyo alimchezea beat nyingi za hip hop, ambazo Joh alimweleza kuwa anazo kibao kwenye maktaba na kwamba angependa kupata ladha mpya.

“Kwahiyo nikamuomba apige beat zake kama marhumba fulani ambayo mtu anaweza akachana,” amesema Joh.

Mweusi huyo anadai hata producer huyo alishangaa uchaguzi wa beat zake japo anadai alikuja kumwelewa baada ya kuurekodi.

Joh anadai kuwa wazo la jina la wimbo huo lilikuja baada ya kugundua kuwa Chidinma alikuwa akiweza kushika vitu alivyoambiwa kwa haraka na kuiona kuwa ingekuja kuwa ‘perfect combo.’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents