Habari

Joto laleta maafa Sudani Kusini

Serial ya Sudan Kusini imeamuru kufungwa kwa seule zote kwa muda usiojulikana kwa sababu ya wimbi la joto ambalo linaweza kusababisha joto kuongezeka hadi 45C (113F).

Mamlaka ya afya na elimu pia iliwataka wazazi kuwazuia watoto wao kucheza nje kwa muda mrefu, wakisema joto hilo linaweza kudumu kwa muda.

Tayari kuna visa vya vifo vinavyohusiana na joto kupita kiasi vinavyoripotiwa, mamlaka ilisema katika taarifa yao.

Walisema kuwa nchi ilikuwa ikipitia  vipindi vilivyoongezwa vya hali joto ya mchana na usiku ambayo inaleta mkazo mwingi wa kisaikolojia kwenye mwili wa mwanadamu.

Shule yoyote itakayopatikana imefunguliwa kuanzia Jumatato ya leo 18 March 2024 itaondolewa usajili wake, mamlaka ilionya.

Wiki iliyopita takribani watoto 15 waliripotiwa kufariki kutokana na homa ya uti wa mgongo na magonjwa mengine yanayohusiana na joto, kulingana na wizara ya afya.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents