Habari

Juma Nature kuanzisha ‘Juma Nature Foundation’ ili kusaida wasiojiweza, na biashara ya ndala kuanza soon…

Msanii mkongwe wa muziki nchini Juma Kassim aka Juma Nature amesema yupo katika hatua ya mwisho ya kufungua ‘Juma Nature Foundation’ itakayokuwa ikisaidia watu wasiojiweza na watoto yatima.

Juma-Nature

Juma Nature ambaye ni msanii na mfanyabiasha ameiambia bongo5 kuwa kila kitu kipo safi katika hatua za kufungua foundation hiyo, pia biashara yake ya ndala inakaribia kuanza baada ya makontena kutoka China kuwasili bandarini.

“Unajua muziki umenitoa mbali sana sasa nikisema nitoe shukurani sijaona wa kumpa zaidi ya watoto yatima na wasio jiweza, kwahiyo nitafanya kwa moyo mmoja kama watu walivyoweza kunisaidia mimi kuweza kufika hapa nilipo. Biashara yangu ya ndala siku si nyingi itaingia sokoni,tayari makontena ya ndala yapo bandarini tukiyachukua na biashara inaanza pia tunafanya na biashara ya t shirt ambayo kwasasa inafanya poa sana,” Alisema Nature.

Kwa upande wa msimamizi wa shughuli za Nature, Issa Uwasa amesema wanamalizia mambo ya usajili wa Foundation hiyo ili waanze kurudisha fadhila kwa jamii.

“Unajua kuwa na foundation kwa msanii kama Nature ni kitu cha muhimu sana, anazunguka sehemu mbalimbali za Kimataifa, kama ataweza kutumia jina lake vizuri basi na watoto yatima na wasio jiweza watanufaika pia, kwahiyo yote ni kuonesha ni jinsi gani wasanii wana umuhimu kwa jamii zao” Amesema Uwasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents