Burudani

Kala Jeremiah aanza ku record remix ya ‘Wale Wale’, awashirikisha Nature, Young Killer na Ney Lee

Msanii wa Hip Hop Kala Jeremiah amesema leo ameanza ku record remix ya wimbo wake mpya ‘Wale Wale’ ambayo atawashirikisha Juma Nature,Young Killer na mwanadada Ney Lee.

page

Akizungumza na bongo5 leo Kala amesema ameona kuna umuhimu mkubwa wa kufanya remix ya wimbo huo kwani ni wimbo ambao unajikita kwenye maswala ya kijamii ndiyo maana unafanya vizuri.

“Unajua ‘Wale Wale’ ni wimbo ambao unazungumzia maisha ya Watanzani, kama kawaida ya nyimbo zangu nyingi ambazo nimefanya zinazungumzia mambo ya kijamii sana, kwahiyo nikaona kuna umuhimu wa kufanya remix yake,ndiyo maana nimeingia studio kufanya remix hiyo ambayo ndani yake kutakuwa na Juma Nature, Ney Lee na Young Killer”

Kala aliongeza kwa kuelezea umuhimu wa wasanii wote alioamua kuwashirikisha katika remix hiyo,

“Juma Nature ana nafasi kubwa sana katika muziki wetu hapa Tanzania, ni kama mkongwe wa muziki wetu na nyimbo zake nyingi zinazungumzia maswala ya kijamii, kwahiyo nikaona ni mtu muhimu akiwepo katika remix yangu. Pia Young Killer ni mtoto wa nyumbani Mwanza toka yupo dogo ninamuona kwahiyo uwezo wake naujua, nakumbuka wakati nazindua video yangu ya Dear God niliwaambia watu wa redio Mwanza kwamba Young Killer ni msanii wa kumwangalia sana, yani anaweza sana,Kwa upande wa Ney Lee sitaki kusema lolote nadhani watu wanatambua uwezo wake,kwaiyo wadau wasubirie kitu kitamu kinakuja”, Alisema Kala.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents