Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMahojiano

Justin Bieber kuuza haki miliki ya nyimbo, kwa Tanzania inawezekana??

Justin Bieber amekuwa msanii pekee wa kizazi chao kuuza haki miliki za nyimbo zake kwa asilimia 100 kwa kampuni kutoka nchini Uingereza ya Hipgnosis Songs Capital kwa kiasi cha $200m sawa na Tsh bilioni 467.

Hatua hiyo inamaanisha kuwa Hipgnosis itapokea malipo kila wakati wimbo wanaomiliki sehemu yake unapochezwa hadharani.

Wasanii wanazidi kuuza hisa katika kazi zao kwa fedha za muziki – ikiwa ni pamoja na Justin Timberlake na Shakira, ambao pia wamepiga dili na Hipgnosis.

Lakini hali hiyo ni ya kawaida zaidi kati ya wasanii wakubwa. Katika miaka miwili iliyopita, nguli wa muziki Bob Dylan na Bruce Springsteen wote waliuza haki za katalogi kwa Sony.

Kampuni ya Hipgnosis imenunua haki zote za Bieber ikiwemo album zake (6), EP (2) na singels zaidi ya 70 (Publishing copyrights, Master Recordings na neighboring rights)

Mbali naa Justin Bieber kufannikisha hili msanii mwinngine ni Dr. Dre ambaye naye yupo kwenye hatua za mwanzo za kutaka kuuza haki za nyimbo zake zote.

Wasanii wa Marekani wamegundua nini??

Unahisi jambo kama hili linawafaa wasanii wetu wa Tanzania?? kama nndio muziki wetu unalipa kiasi kwamba msanii auze haki miliki za nyimbo zake??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents