Burudani

Jux kufungua duka maalum kuuza bidhaa za ‘African Boy’

Jux amepania kuifanya clothing line yake, African Boy kuwa kubwa si tu Tanzania bali, Afrika nzima.

12959967_212934415754393_1415712405_n

Muimbaji hugo wa ‘Looking For You’ amesema siku za usoni amepanga kufungua duka ambalo litakuwa likiuza bidhaa za African Boy tu.

Zaidi ya t-shirts, Jux amesema kwa sasa kuna mabegi, ribbon, sneakers, kofia, makava ya simu, na vingine vinakuja. Akiongea na Lil Ommy kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, Jux amesema sneakers zake zitaingia sokoni baada ya takriban wiki mbili.

Amesema kwa sasa vinatengenezwa kiwandani. Hata hivyo amedai ilimchukua muda kuweza kuja na design ya viatu vyake na kwamba ana ndoto kubwa na mradi huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents