Habari

Kagera: akamatwa na Polisi akishiriki mapenzi na mbuzi

Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera linamshikilia Emmanuel Zakaria (38) mkazi wa Lusahunga wilayani Biharamulo kwa tuhuma za kumkuta akishiriki mapenzi na Mbuzi katika kichaka.

Kwa mujibu wa Eatv.tv. Kamanda wa polisi mkoani Kagera Awadhi Haji, amesema kuwa baba huyo alikutwa na mpita njia akifanya kitendo hicho Oktoba 24 mwaka huu saa 09:00 Alasiri, ambaye alipiga kelele zilizosababisha wananchi kufika haraka na kumkamata.

“Wananchi walimkuta akiwa uchi akimfanyia Mbuzi kitendo hicho, walimkamata na kumkabidhi polisi, tunaye na tunaendelea kumhoji, lakini pia atapimwa afya ya akili ili kubaini kama hana tatizo ya ugonjwa wa akili na baadae hatua za kisheria zitafuta” amesema Kamanda Awadhi

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents