Habari

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji awaapisha Makamishna wapya

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye amewaaapisha Makamishna wapya jana katika hafla fupi iliyofanyika Makao makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimvisha cheo Kamishna wa Divisheni ya Operesheni Billy Mwakatage,wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.

Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji:


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimvisha cheo Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya Moto, Jesuald Ikonko wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimsikiliza Msemaji wa Jeshi hilo Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi,akitoa utambulisho mfupi wa Makamishna wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.


Kamishna wa Divisheni ya Oparesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akila kiapo cha Utii mbele yaKamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye,wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.


Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya Moto wa Jeshi la Zimamoto na, Jesuald Ikonko, akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye(watatukulia), akiwa katika picha na Kamishna wa Utawala na Fedha, Michael Shija (wapili kulia), Kamishna wa Oparesheni Billy Mwakatage (kushoto) na Kamishna wa Usalama dhidi ya Moto, Jesuald Ikonko (kulia) wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents