Kanisa la Beyonce laanzishwa Marekani, linaitwa ‘The National Church of Bey’

Si tu anavutia mashabiki wengi duniani kote, ‘King Bey’ (kama anavyojiita mwenyewe) sasa ana waumini wa kanisa lenye jina lake.

beyonce-time-100-11

Kanisa hilo limepewa jina “The National Church of Bey” na limeanzishwa na kundi la marafiki ambao hukusanyika kila Jumapili kuimba nyimbo za Beyonce kutukuza dini iitwayo ‘Beyism’ ambayo inahusiana na Beyonce. Mwanzilishi wa kanisa hilo, Pauline John Andrews amesema anafedheheshwa na jinsi umma unavyoshindwa kutambua uwepo wa mtu mtakatifu kama Beyonce.

Kwa mujibu wa taarifa, kanisa hilo limechapisha hadi biblia ‘Beyble’ na itaanza kupatikana mtaani bure hivi karibuni. Kundi hilo linatarajia kujenga kanisa lake na litajitanua zaidi hadi nje ya Atlanta, lililokoanzia.

Kanisa likikamilia, wamepanga kumwalika staa huyo ili azungumze.

Related Articles

Back to top button