Burudani

Kanye West apanga kumnunulia Kim Kardashian hekalu, Kim asema anataka kumzalia watoto 6

Kanye West hataki kumnunulia Kim Kardashian nyumba ya kawaida, anataka kumnunulia hekalu. Yeezus anaamini hiyo ndio inaweza kuwa zawadi mahsusi kwa mchumba wake huyo aliyemzalia mtoto wa kike, North.

Kanye West Show : Front Row - Paris Fashion Week Womenswear Fall/Winter 2012

Ili kuhakikisha hekalu hilo linapatikana, Ye ametoa kazi kwa wafanyakazi wake kulisaka barani Ulaya. ‘Hakuna kitu kizuri sana kwa Kim! Mke wangu anastahili kutendewa kama malkia, na hicho ndicho nakwenda kumfanyia,” chanzo kimoja kilimnukuu Kanye.

Kabla ya hekalu, Kanye anamalizia mjengo wao mwingine wa dola milioni 11 uliopo Bel Air, Los Angeles. Nyumba hiyo kwa sasa inafanyiwa ukarabati ambapo imewekewa vitanda vyenya gharama ya $185,000 pamoja na vyoo vilivyozungushiwa dhahabu $800,000.

Wakati huo huo Kim amemuambia Ellen DeGeneres kwenye kipindi chake kuwa anataka kuwa na watoto sita baada ya kuona raha ya kuwa na mtoto kutokana na kumzaa North.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents