Michezo

Kauli tata ya Kichuya kwa Kelvin Yondani ‘kumtemea mate mwenzio ni kukosa ustaarabu, tuache ushamba’

Winga wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania, Shiza Ramadhani Kichuya ameonekana kutopendezwa na kitendo cha mchezaji wa Yanga, Kelvin Yondani kumtemea mate beki, Asante Kwasi wakati walipokuwa kwenye mchezo wao wa watani wa jadi hapo jana siku ya Jumapili na kumalizika kwa ushindi wa bao 1 – 0.

 

 

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram, Kichuya ameandika kuwa mchezo wa mpira siyo vita hivyo kitendo cha kumtemea mate mwenzio ni kitendo cha kukosa ustaarabu.

”Mpira sio vita,kumtemea mwenzio mate ni kukosa ustaharabu na utu tukemee hii,tuache ushamba kuna maisha baada ya mpira,” amesema Kichuya.

Kwenye mchezo huo uliyokuwa na upinzani wa hali ya juu vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba ilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 1 – 0 lililofungwa na beki wake, Erasto Nyoni kwa njia ya kichwa dakika 37 ya kipindi cha kwanza cha mchezo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents