Burudani

KBC wa Kwanza Unit: Hip hop ni utamaduni unaobadilika kulingana na maeneo, trap pia ni hip hop

Kumekuwepo na mjadala mkubwa sana kuhusiana na mabadiliko ya hip hop na kama aina fulani ya muziki wa sasa inaweza kuwa sehemu ya utamaduni huo.

hip-hop-graffiti

Mtangazaji wa kipindi cha Ladha 3600 cha EFM, Jabir Saleh amekuwa akitoa jukwaa kwa wadau wa hip hop nchini kuelezea mtazamo wao kuhusiana na dhana hiyo. Awamu hii amezungumza na rapper mkongwe aliyekuwa member wa kundi la zamani, Kwanza Unit, Kibacha aka KBC.

Haya yalikuwa maoni yake:

Hip hop inakua, haikai sehemu moja. Na inavyozidi kukua, kila kitu kinakuwa na branches nyingi, kwamba hata sound yenyewe haiko moja tena, sound ziko nyingi, inategemea na upande gani watu wanaishi. Ukisema Marekani, ukienda West Coast utakuta kuna sound nyingine, ukienda East Coast kuna sound nyingine, ukienda south kuna sound nyingine, zote ni hip hop, pamoja na zile ambazo kuna mdogo wangu mmoja tulikuwa tunabishana sana kilingeni siku moja sasa yeye akawa anasema ‘Designer sio hip hop’ lakini ni kwasababu yeye hampendi hip hop na anajua mtu kama mimi simpendi Designer yaani kwamba zile beat trap na nini akawa anasema kwamba zile sio hip hop. Sio kweli, zote ni hip hop

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents